Flamingo e.V.

Mitandao ya wakimbizi kwa wanawake na watoto


Flamingo e.V. ni shirika yasio na faida na ina makao yake hapa Berlin na inasaidia wanawake wakimbizi wakiwa peke yao ama na watoto ama wajawazito. Pia tunahudumia watoto wale hawajaandamana na familia zao bila kujali asili yao ama watokako.

 

Wanachama wetu ni wanawake ambao kwa sehemu nyingi wana historia ya uhamiaje . Katika majira ya joto ya 2015 tulianza chama cha kutekeleza malengo yetu kwa ufanisi zaidi.

 

Uhuru, kujitegemea, ushiriki wa jamii na kuimarisha haki za wanawake na watoto wakimbizi.

 

Sisi zote tumekuwa tukifanya kazi Katika nyanja mbali mbali kwa miaka na tuna uzoefu katika uharakati wa siasa, shirika la kibinafsi na msaada kwa wakimbizi.